Home Uncategorized KOCHA NAMUNGO AOMBA DAKIKA 270 KUIMARISHA KIKOSI

KOCHA NAMUNGO AOMBA DAKIKA 270 KUIMARISHA KIKOSI


 HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa kwa sasa anahitaji mechi zaidi ya tatu ambazo ni dakika 270 ili kurejesha makali ya kikosi hicho ambacho kinakwenda mwendo wa kusuasua kwa msimu wa 2020/21.

Namungo FC walianza kwa kasi msimu wa 2019/20 ikiwa ni msimu wao wa kwanza baada ya kupanda Ligi Kuu Bara na ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya nne na pointi 64.Msimu wa 2020/21 kikiwa kimecheza mechi 7 kimepoteza nne na kushinda tatu na pointi zake ni tisa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa muda mfupi ambao aliupata kwa ajili ya maadalizi ya kikosi unaiponza timu hiyo kupata matokeo chanya jambo ambalo linahitaji muda zaidi.

“Hatukuwa na maandalizi mazuri mwanzo mwa ligi hasa hili lipo wazi na kwa namna ambavyo kikosi kinakwenda bado tunahitaji muda zaidi. Siwezi kuwalaumu wachezaji kwani wanapambana hivyo baada ya mechi tatu ama nne kikosi kitakuwa kimerejea kwenye ubora.

“Ushindani ni mkubwa hilo lipo wazi lakini wachezaji bado wanapambana, tulianza na ushindi kwenye mechi yetu ya mwanzo na kwa mwendo tuliona kwa sasa sio mbaya sana hasa ukizingatia kwamba hata ugenini tunapata matokeo,” amesema Thiery.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA ATAJA SABABU YA MAKOCHA KUWA NA PRESHA