Home Uncategorized HAZARD AFUNGA BAO LAKE LA KWANZA NDANI YA REAL MADRID

HAZARD AFUNGA BAO LAKE LA KWANZA NDANI YA REAL MADRID

 


EDEN Hazard ingizo jipya ndani ya Real Madrid amefunga bao lake la kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kujiunga na timu hiyo akitokea Klabu ya Chelsea. 

Hazard alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penalti dakika ya 7 huku lile la pili likiwa ni la kujifunga kutoka kwa mchezaji wa Inter Milan,  Achraf Hakimi dakika ya 59.

Inter Milan ilikubali kufungwa mabao 2-0  ikiwa nyumbani,  Uwanja wa San Siro na kuifanya ipoteze jumla ya mechi mbili na kuwa na sare mbili kati ya mechi nne ilizocheza ndani ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Kwenye msimamo wa kundi B ipo nafasi ya nne na Madrid wao wapo nafasi ya pili na pointi zao kibindoni ni 7.


Tangu ajiunge na Madrid hajawa kwenye ubora wake kutokana na kusumbuliwa na majeraha jambo ambalo limekuwa likimuweka nje ya uwanja muda mrefu.

SOMA NA HII  SIMBA YAPIGA 4G JKT TANZANIA, JAMHURI