Home Uncategorized YANGA YAIPA NGUVU NAMUNGO KIMATAIFA

YANGA YAIPA NGUVU NAMUNGO KIMATAIFA

 


KOCHA mkuu wa Namungo, Hemed Morroco amesema kuwa sare waliyoipata dhidi ya Yanga ni maandalizi tosha kuelekea katika mchezo wa Kimataifa dhidi ya Al Rabita FC ya Sudan Kusini.

 

Namungo ambao wanashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho wanatarajia kuwa wenyeji wa Al Rabita katika mchezo unaotarajia kufanyika wikiendi hii katika Uwanja wa Azam Complex jijini Dar.

 

Kocha huyo amesema kuwa ukiachana na matokeo ya sare waliyoyapata dhidi ya Yanga, kucheza dhidi ya timu hiyo kwao yanakuwa maandalizi mazuri kuelekea kwenye mchezo wa kwanza wa michuano hiyo.

 


Sare hiyo ilipatikana Uwanja wa Mkapa Novemba 21 ambapo timu zote ziligawana pointi mojamoja na shujaa wa mchezo alikuwa ni Metacha Mnata ambaye aliokoa penalti ya Bigirimana Blaise mwenye mabao manne.


Kocha huyo amesema:- “Yanga ni timu ya hadhi ya michuano ya kimataifa na hivyo ukiachana na matokeo ambayo tuliyapata ya sare ya bao 1-1, tunachokiangalia zaidi ni maandalizi kuelekea mchezo wetu.

 

“Hakika Yanga imetupa changamoto nzuri ambayo naamini itatusaidia kuelekea katika mchezo wetu ujao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Rabita FC,” .


Kocha huyo amerithi mikoba ya Hitimana Thiery ambaye alifutwa kazi Novemba 18 alikuwa hana timu baada ya kuachana na Mbao FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.

SOMA NA HII  HASHEEM IBWE AWAOMBA WATANZANIA WAENDELEE KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA