Home Uncategorized KLOPP APATA HOFU KUIKABILI MANCHESTER CITY

KLOPP APATA HOFU KUIKABILI MANCHESTER CITY

 


KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp amesisitiza kuwa leo atakuwa na kazi ngumu kwani kucheza na Manchester City huwa kuna ugumu kati yao.


 Leo Jumapili,Novemba 8 Man City itavaana na Liverpool kwenye Uwanja wa Etihad ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu England.

 

Msimu uliopita kwenye Uwanja wa Etihad, Man City aliibuka na ushindi wa mabao 4-0, huku walipokutana Anfield, Liverpool alishinda 3-1.


“Aina ya mechi hii huwa ni ngumu, lakini pia huwa nafurahia mchezo wa namna hii kwani huwa nafanya maandalizi lakini mambo yanakuja kuwa magumu yaani kukutana na Man City ni mechi ngumu kwangu kwenye soka kuliko zote.

 

 

“Inakuwa mechi nzuri nimefanya maandalizi lakini unakuta napoteza au wakati mwingine nashinda ila ndiyo soka na inabidi tu ufurahi sababu huna namna.


“Pamoja na kupata changamoto na kujiandaa tumekuwa hatuchezi mechi nyingi ambazo zinakuwa na ubora kama ule wa Man City kwani timu hii imekuwa na ubora wa kipekee.

 

“Ila pia haijalishi kama tunacheza nyumbani au ugenini cha msingi sisi tunatakiwa kuwa imara na kucheza soka safi licha ya kuwepo kwa ugumu,” alisema Klopp.

SOMA NA HII  TAIFA STARS NA KIBARUA KINGINE KESHO UWANJA WA MKAPA