Home Uncategorized KOCHA YANGA ATOA TAMKO KUHUSU POINTI MOJA

KOCHA YANGA ATOA TAMKO KUHUSU POINTI MOJA

 


CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kupata pointi moja mbele ya Gwambina ni jambo jema kwani wachezaji wake walijituma kusaka ushindi mambo yakagoma.


 Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Gwambina Complex ulikamilika kwa dakika 90 kwa timu zote kutoshana nguvu na kugawana pointi mojamoja.


Licha ya kupata sare hiyo Yanga iliwashusha nafasi ya kwanza Azam baada ya kufikisha pointi 23 kibindoni baada ya kucheza mechi 9 huku Azam FC ikiwa nafasi ya pili na pointi 22 nayo pia imecheza mechi tisa.


Tayari kimeshatia timu ndani ya Bongo na kuingia kambini jumla kikianza maandalizi ya mechi dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Novemba 7, Uwanja wa Mkapa.


Kaze amesema:”Kupata pointi moja ugenini sio mbaya kwa sasa akili zetu ni kwenye mchezo wetu dhidi ya Simba, imani yetu tutafanya vizuri na tutapambana kupata pointi tatu muhimu.”

SOMA NA HII  LUSAJO MTAMBO WA MABAO NDANI YA NAMUNGO UNAOHUSISHWA KUJIUNGA YANGA