Home Uncategorized MSHAMBULIAJI WA SIMBA AIPIGIA HESABU YANGA

MSHAMBULIAJI WA SIMBA AIPIGIA HESABU YANGA

 


IMEELEZWA kuwa nyota wa Simba Charles Ilanfya yupo kwenye hesabu za kutua ndani ya Klabu ya Yanga kwa mkopo.


Habari zinaeleza kuwa hatua hiyo imefikia baada ya nyota huyo kuomba ruhusa ya kusepa kwa mkopo ndani ya timu hiyo inayonolewa na Sven Vandenbroeck kutokana na ugumu wa namba.


Akiwa Simba ambapo alijiunga hapo akitokea Klabu ya KMC amecheza mchezo mmoja wa Ligi Kuu Bara na hakuyeyusha dakika zote 90 ilikuwa dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela.


Nyota huyo ameomba kurejea KMC ikiwa mambo yatakuwa magumu basi anaweza kwenda Yanga ambao walikuwa kwenye hesabu za kuipata saini yake msimu wa 2018/19 kabla hajaibukia KMC zama zile akiwa ndani ya Mwadui FC.


“Ilanfya ameona kwamba mambo ni magumu ndani ya Simba hivyo ameomba kuondoka akapate nafasi ya kucheza kwa kuwa hapati ndani ya kikosi hiki.


“Timu ya kwanza anayofikiria ni KMC na ya pili ni Yanga ambao walikuwa wanahitaji saini yake zamani, ” ilieleza taarifa hiyo.


Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa bado hawajapata taarifa kuhusu nyota huyo kurejea ndani ya KMC.

SOMA NA HII  KOCHA MBEYA CITY AMCHANA KIPA WAKE, HAPEPESI MACHO - VIDEO