Home Uncategorized SURE BOY: AZAM FC TUNATAKA KOMBE LA LIGI KUU BARA

SURE BOY: AZAM FC TUNATAKA KOMBE LA LIGI KUU BARA


 KIUNGO wa Azam FC, Aboubakar Salum ‘Sure Boy’, amebainisha wazi kuwa licha ya kupoteza pointi tano kati ya sita walizotakiwa kupata kwenye mechi zao mbili za Ligi Kuu Bara, kitendo hicho hakiwafanyi watoke kwenye mstari wa kugombea ubingwa.

 

Kiungo huyo ameongeza kuwa wataendelea kupambana na kufikia ndoto yao hiyo kwa msimu huu kutokana na mechi nyingi ambazo wamezibakisha mkononi.

 

Azam FC kwa mara nyingine Ijumaa iliyopita walishindwa kuvuna pointi tatu baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na JKT Tanzania. Kabla ya hapo walifungwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar.

 

Sure Boy amesema kuwa licha ya kufanya vibaya kwenye mechi hizo lakini suala hilo haliwakatishi tamaa ya kuwa mabingwa kwa msimu huu.

 

“Haya ni matokeo ya mpira na inaonyesha ligi ilivyo na ushindani lakini hayatufanyi kutoka kwenye malengo ambayo tumejiwekea kwa msimu huu.

 

“Tunataka kutwaa ubingwa na tuna mechi nyingi mkononi, hivyo tutapambana kwa ajili ya kushinda na kufanikisha hili ambalo tunalitaka kwa msimu huu,” alimaliza Sure Boy.

SOMA NA HII  ROSTAM AWA MFALME YANGA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here