Home Uncategorized YANGA YAFUNGUKIA USAJILI WA MAJEMBE HAYA MAWILI

YANGA YAFUNGUKIA USAJILI WA MAJEMBE HAYA MAWILI


UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa mpango wa kuboresha kikosi chao kuelekea kwenye dirisha dogo ambalo linatarajiwa kufunguliwa Desemba 15 upo mikononi mwa Kocha Mkuu, Cedric Kaze ambaye ana kazi ya kuandika ripoti.

Habari zimekuwa zikieleza kuwa Yanga chini ya Kaze inahitaji kuboresha sekta ya ushambuliaji ambayo imekuwa inasumbuliwa na ubutu wa kufunga mabao pamoja na kiungo mshambuliaji atakayekuwa na kazi ya kutengeneza mipango kwa wafungaji kama ilivyokuwa zama za Ibrahim Ajibu ambaye yupo Simba.

Majina ambayo yanatajwa kuibukia ndani ya kikosi hicho ni pamoja na staa wa timu ya Taifa ya Tanzania, Adam Adam ambaye ni mshambuliaji na Gerald Mdamu wa Biashara United ambaye ni kiungo mshambuliaji.

Adam amekuwa kwenye ubora wake msimu wa 2020/21 ambapo amefunga jumla ya mabao sita na kutoa pasi moja ya bao ndani ya Klabu ya JKT Tanzania huku Mdamu wa Biashara United dili lake lilikwama msimu uliopita alipokuwa akicheza ndani ya Mwadui FC.

Akizungumza na Saleh Jembe, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa mpango wa kuboresha kikosi upo kuelekea dirisha dogo lakini unasubiri ripoti kutoka kwa Kaze.

“Kuna majina ambayo yanatajwa ikiwa ni pamoja na Adam na Mdamu, hawa wote ni wachezaji ndio maana wanapewa nafasi kwenye timu zao lakini ili mchakato huo ukamilike ni lazima tufuate ripoti ya kocha inasema nini hivyo ni jambo la kusubiri,” amesema Mwakalebela.

SOMA NA HII  CHAMA CLATOUS AFUNGUKIA ISHU YAKE YA KUIBUKIA YANGA