Uncategorized

MRITHI WA AKONOAKONO KUSAINI DILI LA MWAKA MMOJA AZAM FC

admin December 22, 2020 7:47 pm


 NYOTA wa FC Lupopo Mpiana Moziz ametua ndani ya Bongo kwa ajili ya kumalizana na mabosi wa Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu George Lwandamina. 

Mshambuliaji huyo amekuja leo Desemba 22 akitokea nchini Congo na kesho Desemba 23 anatarajiwa kufanyiwa vipimo ambapo akifuzu atasaini dili la mwaka mmoja.

Amekuja kuchukua nafasi ya aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo Thiery Akono raia wa Cameroon ambaye ameuzwa na Klabu ya Azam FC na kuibukia nchini Malysia kwenye Klabu ya Negeri Sembilan.


Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa mpango mkubwa ni kuona kwamba kikosi kinarejea kwenye ubora wake kwa kupata wachezaji makini.


“Tumemleta Moziz ndani ya Bongo ambapo mpango wetu ni kumfanyia vipimo vyote pamoja na kucheki utimamu wake ikiwa kila kitu kitakuwa sawa atasaini mkataba wa mwaka mmoja ndani ya Azam FC,”.

TANZANIA YAISHIA NAFASI YA PILI FAINALI YA CECAFA U 17 MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply