Home Uncategorized JKT TANZANIA YASIMAMISHA USAJILI WA KMC

JKT TANZANIA YASIMAMISHA USAJILI WA KMC


 UONGOZI wa KMC umesema kuwa hesabu zao kwa sasa ni kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania unaotarajiwa kuchezwa Desemba 23, Uwanja wa Jamhuri.

KMC imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Ihefu FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Highlands jana, Desemba 19.

Bao pekee la ushindi kwa Ihefu FC inayonolewa na Zuber Katwila lilipachikwa kimiani na Joseph Kinyonzi dakika ya 9 na kuwafanya wabaki na pointi tatu jumlajumla kwenye mchezo huo.

Hivyo maandalizi ya mchezo wa JKT Tanzania dhidi ya KMC umesimamisha kwa muda mpango wa usajili wa timu hiyo.


Ushindi huo unaifanya Ihefu kufikisha jumla ya pointi 13 baada ya kucheza mechi 16 ipo nafasi ya 16 kwenye msimamo.


KMC ipo nafasi ya 8 baada ya kucheza mechi 15 kibindoni ina pointi 21.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa kwa sasa wameweka kando mipango ya usajili mpaka watakapomaliza hesabu mbele ya JKT Tanzania.

“Tunajua kamba ni wakati wa dirisha dogo la usajili ila ngoja tuweke kando kwanza masuala hayo mpaka pale ambapo tutamaliza mchezo wetu dhidi ya JKT Tanzania.


“Baada ya hapo tutaweka wazi mipango yetu kuhusu usajili na kila kitu kitakuwa sawa, mashabiki wazidi kutupa sapoti,” amesema.


Dirisha dogo la usajili limefunguliwa Desemba 16 na linatarajiwa kufungwa Januari 16.

SOMA NA HII  MESSI ANATAKA KUSEPA BARCELONA