Home Uncategorized KATWILA: DIRISHA DOGO TUTAFANYA USAJILI UTAKAOTUBEBA

KATWILA: DIRISHA DOGO TUTAFANYA USAJILI UTAKAOTUBEBA


 KOCHA Mkuu wa Ihefu FC ya Mbeya inayotumia Uwanja wa Sokoine, Zuber Katwila amesema kuwa watatumia dirisha dogo kufanya maboresho ya kikosi hicho ili kirejee kwenye ubora.


Ihefu imekuwa kwenye mwendo wa kusuasua ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 ambapo tatizo kubwa kwa mujibu wa Katwila lipo kwenye safu yake ya ushambuliaji na ulinzi.


Ikiwa imecheza jumla ya mechi 13 safu yake ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao matatu ikiwa na pointi sita nafasi ya 18.


Ndani ya dakika 1,620 ina wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 540 jambo ambalo linampa wakati mgumu Katwila aliyeibukia ndani ya Ihefu akitokea Klabu ya Mtibwa Sugar.


Katwila ambaye mchezo wake wa kwanza kukaa benchi alipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC Uwanja wa Sokoine amesema bado kuna namna yakufanya.


“Vijana wanacheza kwa juhudi wanakosa uzoefu na namna ya kumalizia nafasi ambazo wanazipata ndani ya uwanja.


“Kuelekea dirisha dogo wapo wachezaji ambao tumeanza kuzungumza nao jambo ambalo litatufanya tuwe imara, kwa sasa tutapambana kuwa imara mashabiki wazidi kutupa sapoti,” amesema.


SOMA NA HII  NYOTA SABA WA NAMUNGO FC WA KIKOSI CHA KWANZA KUIKOSA FAINALI YA LEO MBELE YA SIMBA