Home Uncategorized MO SALAH, KLOPP, MESSI,RONALDO WAWANIA TUZO YA KARNE

MO SALAH, KLOPP, MESSI,RONALDO WAWANIA TUZO YA KARNE


 LIONEL Messi, Cristiano Ronaldo, Ronaldinho na Mohamed Salah wanawania tuzo ya mchezaji bora wa karne ya 21 kwenye Tuzo za Soka za ulimwengu (Dubai Globe Soccer Awards), baada ya kupigiwa kura milioni nane ulimwenguni kote kutoka nchi zaidi ya 230.

 

Cristiano, Messi na Lewandowski pia wameteuliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa 2020. Pamoja na tuzo za mtu binafsi, kutakuwa pia na tuzo kwa klabu bora ya karne ya 21, ambapo miamba ya Misri, Al Ahly, wataminyana na Bayern Munich, Barcelona na Real Madrid kuwania tuzo hiyo ya klabu bora ya karne ya 21.

 

Tuzo hizi zimekuwa zikitolewa kila mwaka tangu mwaka 2010, ambapo tuzo zimekuwa zikitolewa kwa kocha bora, timu bora na wakala bora. Tuzo za mwaka huu zitatangazwa Desemba 27, 2020,  na ni kwa mara ya kwanza washindi watapatikana kwa kupigiwa kura na mashabiki.

 

Orodha ya tuzo zinazowaniwa kwa upande wa tuzo za ubora kwa Karne ya 21 hii hapa:

  • Tuzo mchezaji bora wa Karne: Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Ronaldinho na Mohamed Salah.
  • Tuzo kocha bora wa Karne: Sir Alex Ferguson, Pep Guardiola, Jose Mourinho na Zinedine Zidane.
  • Tuzo klabu bora ya Karne: Al Ahly, Bayern Munich, Barcelona na Real Madrid.
  • Tuzo ya wakala bora wa Karne: Giovanni Branchini, Jorge Mendes na Mino Raiola.

 

Tuzo nyingine zitakazotolewa hiyo Desemba 7, 2020, ni tuzo za ubora kwa mwaka 2020.

  • Tuzo ya mchezaji bora 2020; Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Robert Lewandowski.
  • Tuzo klabu bora 2020 timu zinazowania ni Bayern, Liverpool and Real Madrid.
  • Tuzo kocha bora 2020 wanaowania ni Gian Piero Gasperini (Atalanta), Hansi Flick (Bayern) na Jurgen Klopp (Liverpool).

Mwaka 2019, tuzo ya kocha bora ilienda kwa Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, Cristiano Ronaldo alishinda tuzo ya mchezaji bora na Jorge Mendes alishinda Tuzo ya Wakala Bora wa Mwaka.

SOMA NA HII  PSG WAINGIA ANGA ZA AUBAMEYANG