Home Uncategorized KMC KUIFUATA MTIBWA SUGAR LEO

KMC KUIFUATA MTIBWA SUGAR LEO




TIMU ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC leo, Desemba 10 kinatarajia kuanza safari kuelekea Morogoro kwa ajili ya kuiwahia Mtibwa Sugar.


 Kesho, Desemba 11, KMC inayonolewa na Kocha Mkuu, John Simkoko akisaidiana na Habibu Kondo kitakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu Uwanja wa Jamhuri, Morogoro dhidi ya Mtibwa Sugar.


Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na wanaamini kwamba watapata pointi tatu kwenye mchezo huo.

“Tunawafuata mapema ili kuweza kujiweka sawa na kwenye mchezo huo tunahitaji pointi tatu ndani ya uwanja ili kuzidi kuwa bora.


“Hakuna mechi ambayo kwetu itatushinda kupata matokeo, hata kama tunacheza na timu ya namna gani, ndio mana tunasema Pira Spana, Pira Mapato,Pira Kodi , tunachokihitaji hivi sasa ni ushindi tu na sio vinginevyo,hivyo hata mechi hii ipo ndani ya uwezo wetu, amesema.

Kwenye msimamo KMC ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 21 inakutana na Mtibwa Sugar iliyo nafasi ya 14 na pointi 16.


SOMA NA HII  KOCHA MPYA YANGA AMEFUNDISHA BARCELONA