Home Uncategorized MTAMBO HUU WA MABAO, MBADALA WA SARPONG WAKUBALI KUTUA YANGA

MTAMBO HUU WA MABAO, MBADALA WA SARPONG WAKUBALI KUTUA YANGA


 NYOTA wa timu ya Gwambina FC, Meshack Abraham amesema kuwa yupo tayari kucheza ndani ya kikosi cha Yanga kwa kuwa anaamini katika uwezo wake.


Mshambuliaji huyo mzawa mwenye mabao sita ndani ya Ligi Kuu Bara ambapo aliongoza kikosi chake jana, Desemba 6 kulazimisha sare ya bila kufungana na Azam FC huku akifanya majaribio ya mara kwa mara ambayo yalimsumbua mlinda mlango Benedict Haule.


Ikiwa imefunga jumla ya mabao 12 yeye amehusika kwenye asilia 50 ya mabao hayo na kuifanya timu yake kuwa nafasi ya 10 na kibindoni ina pointi 17.

Meshack amesema :”Mimi ni mchezaji na ninajua kwamba kazi yangu ni kucheza bila mashaka nina uwezo wa kucheza sehemu yoyote hata ikiwa Yanga sina mashaka ninacheza bila tabu.


“Habari nimekuwa nikiskia kwamba nahitajika na Yanga sio hao tu hata Azam pia naambiwa kwamba wanahitaji saini yangu, pale ambapo kutakuwa na ofa nzuri mimi nitasiani,” amesema.


Nyota huyo anatajwa kwenda Yanga ili akaongeze nguvu kwenye safu ya ushambuliaji inayoundwa na Michael Sarpong mwenye mabao manne ndani ya Ligi Kuu Bara.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI