Home Uncategorized NGORONGORO HEROES YAVULIWA UBINGWA WA CECAFA

NGORONGORO HEROES YAVULIWA UBINGWA WA CECAFA

 

Cecafa U 20

FT


 TIMU ya Taifa ya Tanzania chni ya miaka 20, Ngorongoro Heroes leo Desemba 2 imepoteza ubingwa wa mashindano ya Cecafa dhidi ya Uganda kwa kufungwa mabao 4-1.


Mchezo wa leo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa Uwanja wa Black Rhino ulishuhudiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), Wallace Karia ambaye ni Rais pia wa Cecafa.

Mabao ya Uganda yalifungwa na Richard Basangwa dakika ya 12, Steven Sserwadda dk 44 ,Ivan Bogere 61  na Kenneth Semakula 72.

Bao la Tanzania lilifungwa na Abdul.H.Suleiman dk 30 kwa mkwaju wa penalti na kuwafanya Uganda wasepe na taji hilo ambalo lilikuwa mikononi mwa Ngorongoro Heroes.

SOMA NA HII  MASHABIKI NDANDA HAWAAMINI WANACHOKIONA BAADA YA NGASSA KUFANYA YAKE TAIFA