Home Uncategorized YANGA: HATUTAWADHARAU RUVU SHOOTING

YANGA: HATUTAWADHARAU RUVU SHOOTING


HOMA imezidi kupanda kuelekea mchezo  wa Ligi Kuu Bara utakaozikutanisha Klabu za Yanga na Ruvu Shooting siku ya Jumapili.

Tayari wenyeji wa mchezo huo Yanga wamesisitiza kuwa wanataka pointi tatu muhimu kwenye mchezo huo, hivyo hawatawadharau wapinzani wao. 

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa kikosi cha Yanga, Hafidh Saleh amesema wanajua Ruvu Shooting  ni miongoni mwa timu ngumu ndani ya Ligi Kuu Bara kutokana na ubora wa kikosi walichonacho.

“Mbele yetu tuna mchezo mgumu dhidi ya Ruvu Shooting ambao tunatarajia kucheza nao siku ya Jumapili, tunajua utakuwa mchezo mgumu kutokana na umuhimu wa kupata matokeo chanya kwenye mchezo huu hivyo hatuwezi kuidharau Ruvu.

“Tayari kikosi kipo kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huu ambapo tulianza rasmi kambi siku ya Jumanne na taarifa njema kwetu ni kurejea kwa baadhi ya nyota wa kikosi chetu waliokosa mchezo uliopita dhidi ya JKT Tanzania akiwemo, Kibwana Shomari,” .


Yanga imecheza jumla ya mechi 13 ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 31, inakutana na Ruvu Shooting, Desemba 6 Uwanja wa Mkapa.


Ruvu Shooting ipo nafasi ya nne kibindoni ina pointi 23. 

SOMA NA HII  PUMZIKA KWA AMANI MKAPA,TUJIFUNZE KWAKE