Home Uncategorized NYOTA GWAMBINA KUMRITHI DUBE NDANI YA AZAM FC

NYOTA GWAMBINA KUMRITHI DUBE NDANI YA AZAM FC


 MTUPIAJI namba moja wa timu ya Gwambina FC, Meshack Abraham mwenye mabao 6 ameingia kwenye rada za Azam FC ambao kwa sasa wanamsaka mbadala wa mshambuliaji wao  Prince Dube.

Dube ndani ya Ligi Kuu Bara ndani ya Azam FC inayonolewa na George Lwandamina ametupia jumla ya mabao 6 na ana pasi nne za mabao.

Dube kwa sasa yupo kwenye program ya kutibu jeraha lake la mkono alilolipata kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga ambapo Azam FC ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.


Tayari ameanza mazoezi mepesi baada ya kutoka nchini Afrika Kusini ambako alikwenda kufanyiwa matibabu zaidi baada ya kuanza kupewa huduma kwenye ardhi ya Bongo, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Habari zinaeleza kuwa uongozi wa Azam FC umewafuata viongozi wa Gwambina FC ili kuuliza kuhusu kumpata mchezaji huyo.


Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wanahitaji kufanya usajili ila itategemea na ripoti ya mwalimu kupitia mapendekezo yake ya wachezaji ambao anawahitaji.


SOMA NA HII  YANGA YATUA KWA BEKI MRWANDA