Home Uncategorized SAKATA LA KICHUYA SIMBA WAOMBA LIANZE UPYA

SAKATA LA KICHUYA SIMBA WAOMBA LIANZE UPYA

 


NAMUNGO FC imeweka wazi kuwa sababu ya kumtumia mchezaji Shiza Kichuya ambaye ilielezwa kuwa FIFA wamemfungia kucheza kwa muda wa miezi sita na Klabu ya Simba imepigwa faini kwa kumtumia mchezaji huyo kinyume na taratibu za usajili ni kutokana na Simba kuomba shauri hilo lipitiwe upya.


Kichuya alisajiliwa na Simba kwenye usajili wa Januari akitokea Klabu ya Pharco ya Misri ambao wanadai kwamba alikuwa na mkataba wa miaka miwili na alitumia mkataba wa mwaka mmoja jambo lililowafanya wapeleke malalamiko hayo kwa FIFA kulalamikia suala la usajili wa mchezaji huyo.

Ofisa Habari wa Namungo FC, Kindamba Namlia amesema, Kichuya ataendelea kutumiwa na klabu hiyo kwa sababu Klabu ya Simba imeomba FIFA kufanya mapitio upya ya shauri linalomhusu mchezaji huyo.


“Katika taarifa tuliyopewa kuhusu Kichuya inasema, Kichuya anaweza kufungiwa miezi sita endapo Klabu ya Simba itashindwa kulipa faini ndani ya siku 45.


“Mshtakiwa namba moja kwenye shauri lile Shiza Kichuya anaweza kufungiwa miezi 6, mshtakiwa namba mbili Simba SC inaweza kufungiwa kusajili kwa misimu mitatu (madirisha matatu makubwa ya usajili).


“Kwa sasa Simba imeomba mapitio ya hukumu iliyotolewa na FIFA, kwa maana hiyo kila kitu kinaanza upya hadi mapitio yatakapokamilika. Maana yake hata ule muda iliopewa Simba kulipa faini hauangaliwi hadi pale mapitio yatakapokamilika.


“Taarifa itakayotoka baada ya mapitio ndio itafanya kazi.Sisi tunajitahidi kwenda kiwekedi, baada ya kuipata taarifa kuhusu Kichuya mtu wetu wa sheria hakuwepo kwa hiyo tulisubiri hadi asome nyaraka za taarifa tuliyopewa kuhusu Kichuya na atupe tafsiri yake,” .

SOMA NA HII  YANGA IWE JUA IWE MVUA MPAKA KIELEWEKE NA STRAIKA HUYU WA ASEC