Home Uncategorized TANZANIA PRISONS YATAKA KUVUNJA REKODI YA YANGA

TANZANIA PRISONS YATAKA KUVUNJA REKODI YA YANGA


 SALUM Kimenya, beki wa Klabu ya Tanzania Prisons amesema kuwa wanahitaji kuvunja rekodi ya Yanga kumaliza mzunguko wa kwanza bila kufungwa kwa kusepa na pointi tatu watakapokutana.

Prisons ikiwa imecheza jumla ya mechi 17 imekusanya pointi 21 inakutana na Yanga ambayo imecheza mechi 17 ambazo ni dakika 1,530 bila kupoteza ikiwa na sare nne.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kimenya amesema kuwa wanatambua kwamba wapinzani wao hawajapoteza hivyo wapo tayari kutibua rekodi hiyo.

“Tunajua kwamba hawajapoteza hilo lipo wazi ila nasi pia tunahitaji pointi tatu kwa kuwa nafasi ambayo tupo kwa sasa sio nzuri.

“Kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti tupo tayari kwa ajili ya ushindani na tunahitaji kupata matokeo,” amesema.


Mchezo wa leo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Nelson Mandela saa 10:00 jioni.


Walipokutana Uwanja wa Mkapa, Yanga iligawana pointi mojamoja na Prisons kwa kufungana bao 1-1.

SOMA NA HII  SERIKALI YAWAPA ONYO WANG'OA VITI KWENYE DABI YA KESHO