Home Uncategorized VIBALI VYAMKWAMISHA MKATA UMEME SIMBA

VIBALI VYAMKWAMISHA MKATA UMEME SIMBA

 IMEELEZWA kuwa kuchelewa kamilika kwa vibali vya kiungo mkabaji mpya wa klabu ya Simba raia wa Uganda, Taddeo Lwanga ndiyo sababu kubwa ya nyota huyo kuchelewa kuanza majukumu yake mapya ndani ya Simba.

Lwanga alikamilisha usajili wake na kutambulishwa kujiunga na Simba Desemba 2, mwaka huu ambapo alianza mara moja mazoezi na kikosi cha mabingwa hao watetezi lakini mpaka sasa hajacheza mchezo huku kukamilika kwa vibali vyake ikiwa ni kitendawili.

Akizungumzia kuhusu vibali vya Lwanga Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Barbara Gonzales amesema: “Bado tunapambana kuhakikisha tunakamilisha vibali vya kiungo wetu mkabaji, Taddeo Lwanga vinakamilika ili nyota huyo aanze kuitumikia Simba rasmi, tumefikia mahali pazuri katika hilo na ni matumaini yetu kuwa hivi karibuni kila kitu kitakuwa kimekamilika,” 

SOMA NA HII  SABABU YA MCHEZO WA AZAM FC NA SIMBA KUBADILISHIWA UWANJA YATAJWA