Home Uncategorized WATATU YANGA KUTOLEWA KWA MKOPO,WAWILI TAYARI MAMBO SAFI

WATATU YANGA KUTOLEWA KWA MKOPO,WAWILI TAYARI MAMBO SAFI


 CHIPUKIZI wa Yanga kutoka timu B, Adam Kiondo amejiunga na Klabu ya Ruvu Shooting kwa dili la miezi 6.


Kiondo ambaye ni mshambuliaji aliyeanza kupewa nafasi kikosi cha kwanza anakuwa nyota wa pili kutolewa kwa mkopo ndani ya timu za Ligi Kuu Bara.


Mwingine ambaye ametolewa kwa mkopo ambaye ni mali ya Yanga ni mshambuliaji Juma Mahadhi ambaye anapambana kurejesha kiwango akiwa ndani ya Ihefu FC ya Mbeya.


Tayari Mahadhi ameingia kikosi cha kwanza chini ya Kocha Mkuu, Zuber Katwila wakipambana kuinusuru timu hiyo isishuke Daraja kwa msimu wa 2020/21 ambao ni msimu wake wa kwanza. 


Ikiwa imecheza jumla ya mechi 18 imekusanya pointi 13 ikiwa nafasi ya 17 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara. 


Mwingine  watatu ambaye yupo kwenye hesabu za kutolewa kwa mkopo ni Abdulaziz Makame ambaye huenda akajiunga na Polisi Tanzania.

SOMA NA HII  MABEKI HAWA WAWILI WA SIMBA PASI ZAO ZA MWISHO ZILIMDONDOKEA KAGERE