Home Uncategorized YANGA YAZITAKA POINTI TATU ZA IHEFU

YANGA YAZITAKA POINTI TATU ZA IHEFU



UONGOZI wa Klabu ya Yanga umeweka wazi kwamba unahitaji pointi tatu mbele ya Ihefu FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Sokoine.

Yanga ikiwa nafasi ya kwanza inakutana na Ihefu FC ambayo ipo 16 na pointi 13 zote zikiwa zimecheza jumla ya mechi 16 ndani ya Ligi Kuu Bara.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo na wanahitaji pointi tatu muhimu.

“Tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu ila tupo tayari kwa kuwa tunahitaji pointi tatu muhimu kwenye mchezo wa leo,” .

Mtambo wa kutengeneza mabao kwa Yanga ni Yacouba Songne ambapo kwenye mabao 25 amehusika kwenye mabao 7.Amefunga mabao matatu na ana pasi nne za mabao.


Anakutana na Ihefu FC inayonolewa na Zuber Katwila ambaye ametoka kushinda mchezo wake uliopita mbele ya KMC kwa bao 1-0. Yanga pia ilishinda mbele ya Dodoma Jiji kwa mabao 3-1 hivyo leo mchezo utakuwa na ushindani mkubwa.

SOMA NA HII  COASTAL UNION V YANGA WAPIGANA MKWARA HUU