Home Uncategorized AZAM FC WAPANIA KUENDELEZA REKODI

AZAM FC WAPANIA KUENDELEZA REKODI


 UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa mpango wao ni kuendelea kupata matokeo ndani ya uwanja kwa mechi ambazo zimebaki mkononi mwao.

Desemba 31, Azam ilifunga mwaka kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania uliochezwa Uwanja wa Ushirika, Moshi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa kazi kubwa ni kuendelea kufanya vizuri ndani ya uwanja.

“Tupo vizuri na kila mmoja anajua nini kifanyike ndani ya uwanja, ukweli ni kwamba kila mchezaji anatimiza jukumu lake na lengo kupata matokeo.

“Mashabiki wazidi kutupa sapoti ili kuweza kufikia malengo ambayo tupo nayo na bado hatujakata tamaa,” amesema.

Azam FC ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 32 ndani ya Ligi Kuu Bara.   

SOMA NA HII  MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA LEO NDANI YA LIGI KUU BARA