MANCHESTER City imepanga kufanya usajili utakaoishtua Tottenham kwa kumchukua nyota wao Harry Kane kwa mujibu wa ripoti.
Kocha Mkuu, Pep Guardiola yupo kwenye mpango wa kumsaka mbadala wa nyota wake Sergio Arguero ambapo amesema kuwa anamhitaji nyota wa timu ya Taifa ya England Kane ambaye ni nahodha pia.
Kane ni miongoni mwa wachezaji mahiri kwenye nafasi ya ushambuliaji ambapo ameshinda mara mbili kiatu cha ufungaji bora ndani ya Ligi Kuu England jambo ambalo linamuongezea nguvu Guardiola kuhitaji saini yake.
Huenda City ikamshawishi pia pacha wake Son Heung-min ambaye wamekuwa wakifanya naye vizuri ndani ya Ligi Kuu England hivyo Guardiola anawahitaji ili wawe ndani ya Etihad kwa msimu ujao.
Chini ya Kocha Mkuu, Jose Mourinho, Kane ametupia jumla ya mabao tisa huku akitoa jumla ya pasi 10 za mabao hivyo ameonesha kwamba uwezo wake wa kufunga ni zaidi akiwa ndani ya uwanja akiwa amecheza jumla ya mechi 15.
Pia Son Heung-min yeye ametupia jumla ya mabao 11 na pasi nne za mabao akiwa amecheza jumla ya mechi 15.Arguero amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara kwa msimu wa 2020/21 ndani ya Ligi Kuu England.