Home Uncategorized IHEFU YAGOMA KUSHUKA LIGI DARAJA LA KWANZA

IHEFU YAGOMA KUSHUKA LIGI DARAJA LA KWANZA


KIPA namba moja ndani ya Klabu ya Ihefu FC, Deogratius Munish, maarufu kama Dida amesema kuwa anaamini timu hiyo msimu wa 2021/22 itabaki ndani ya Ligi Kuu Bara.

Dida ameibuka ndani ya Ihefu FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Zuber Katwila ambayo imepanda Ligi Kuu Bara msimu huu ikitokea Ligi Daraja la kwanza.

Haijawa na matokeo chanya ndani ya uwanja msimu huu jambo ambalo linaifanya timu hiyo iwe nafasi ya 18 na pointi 13 baada ya kucheza mechi 18.

Kipa huyo ambaye aliwahi kudaka ndani ya kikosi cha Simba na Yanga pia alidaka ndani ya Lipuli FC ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza, alisajiliwa Ihefu kwenye dirisha dogo akiwa ni mchezaji huru.

Nyota huyo amesema:”Bado kuna nafasi kwa wachezaji kuweza kufanya vizuri kwenye mechi zijazo kwa kuwa bado mechi zipo na makosa tutayafanyia kazi.

“Uwepo wa wachezaji wengi ambao wanahitaji kupata matokeo ndani ya uwanja ni nguvu kwa kila mmoja hivyo mashabiki wazidi kutupa sapoti,” amesema.

SOMA NA HII  USIOGOPE RAPHAEL DAUD, TOKA KWENYE GIZA LA DAR ES SALAAM