Home Uncategorized TUNAHITAJI BINGWA WA KWELI LEO KOMBE LA MAPINDUZI, WENYEJI WAJIPANGE

TUNAHITAJI BINGWA WA KWELI LEO KOMBE LA MAPINDUZI, WENYEJI WAJIPANGE


 PONGEZI kwa timu ambazo zimeshiriki Kombe la Mapinduzi kuanzia hatua ya awali ambayo ilikuwa ni ya mtoano na kila timu kuonyesha ushindani mkubwa.

Kwa sasa tayari kila timu imevuna kile ambacho ilikuwa imepanda ndani ya uwanja kwa kuwa matokeo tayari yanajulikana na yapo wazi.

Ipo wazi kwamba kwa msimu wa 2021 kila timu ilikuwa inashindana kwa kusaka matokeo ndani ya uwanja ili kuweza kufikia malengo ambayo walikuwa wamejiwekea ndani ya uwanja.

Jambo la msingi ambalo kwa sasa linapaswa lifanyike ni maandalizi ya wakati ujao baada ya msimu huu kukamilika ambapo leo hitimisho linatarajiwa kuonekana kwa mchezo wa fainali kuchezwa.

Kwa wachezaji ambao walikuwa wakipambana ndani ya uwanja kwenye mechi zao zilizopita bado wanakazi ya kufanya kwa kuwa kazi ya mpira ni ya siku zote.

Wenyeji licha ya kushindwa kutinga hatua ya fainali bado kuna nafasi ya kufanya vizuri wakati ujao na kuanza kufanya maandalizi wakati huu muda bado unaruhusu.

Itapendeza msimu ujao timu ambazo zimeshiriki msimu huu kwa wale wenyeji wakaongeza zaidi juhudi na uwekezaji kwa timu zao ili kuweza kufanya vizuri zaidi ya hapa ambapo wameishia.

Pia kwa mabingwa watetezi nao bado wana kazi ya kufanya wakati ujao kwa kujipanga kwani kushindwa kupata matokeo haina maana kwamba haina uwezo hapana bado kuna nafasi ya kufanya vizuri.

Kutolewa kwenye mashindano kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Simba kusiwatoe kwenye reli Mtibwa Sugar wana kazi ya kufanya kwa ajili ya kuboresha makosa ambayo wameyafanya ndani ya uwanja.

Mpira ni mchezo wa makosa kwa yale ambayo wameyafanya benchi la ufundi lina kazi ya kuyafanyia kazi ili wakati ujao waweze kufikia malengo wanayohitaji kwa kuwa muda unaruhusu kufanya hivyo.

Matokeo ambayo huwa yanatokea ndani ya dakika 90 yatabaki kuwa hivyo daima ila kwa kuwa yametokea basi ni wakati wa kufanyia kazi makosa hayo.

Shukrani kwa mashabiki ambao wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye mashindano haya na nina amini kwamba kwenye fainali pia itakuwa hivyo.

Wote waliokuwa mwanzo wamepata burudani na kupata matokeo ambayo walikuwa wanahitaji uwanjani kwa namna ambavyo timu zao zilikuwa zimejipanga.

SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR YATAJA SABABU YA KUIMALIZA AZAM FC GAIRO

Kwa kuona burudani ambayo ilikuwa inatolewa na timu zao ni fursa ya mwendelezo wao kuendelea kuzipa sapoti timu zao. Wanastahili pongezi katika hilo kwa kuwa muhimu kwa mashabiki kujitokeza.

Burudani ambayo mlikuwa mnaishuhudia kutoka kwa wachezaji imechangiwa pia na ile amshaamsha ambayo ilikuwa inafanyika ndani ya uwanja ninawapa pongezi.

Tukirudi leo ambapo kutakuwa na mchezo wa fainali wa kumjua nani atakayetwaa taji la Kombe la Mapinduzi ni wakati wa kila mchezaji kutimiza majukumu yake uwanjani.

Kuanzia kwa mashabiki watakaojitokeza wazipe sapoti timu zao bila kuchoka kwa kuwa watamjua yule bingwa baada ya dakika 90 kukamilika.

Waamuzi pia ni wakati wa kuendelea kusimamia kwenye sheria 17 na kufanya maamuzi ya haki ni muhimu kuzingatia kwamba kila mmoja anafanya kwa weledi kazi yake.

Kwa kufanya hivyo itasaidia kupatikana kwa bingwa wa haki wa Kombe la Mapinduzi.

Kwa waandaaji pia ni muhimu kuzidi kuboresha mashindano haya ili yazidi kuwa na mvuto kwa kuwa mwanzoni ilikuwa na mvuto mkubwa.

Simba na Yanga hawa ni watani wa jadi na mchezo huu ni mkubwa ambao utafuatiliwa na wengi duniani kwa kuwa ni timu mbili zinakutana kwenye fainali ya heshima.

Kuanzia kwa wachezaji ni muhimu kuweza kufanya kile ambacho kitawapa matokeo mazuri kwa kufuata maelekezo ambayo mmepewa na benchi la ufundi.

Muhimu kuwa makini na kufanya kazi kwa nidhamu ndani ya uwanja kila mmoja afanye kwa moyo bila kutegea ndani ya uwanja.

Hii ni fainali ya pili kwa watani hawa kukutana hivyo kila mmoja anahesabu zake ndani ya kichwa katika kutimiza malengo ambayo yamewekwa na timu hizi mbili.

Utulivu unahitajika kwa kila mchezaji ndani ya uwanja. Kila timu inahitaji ushindi hakuna ambayo inahitaji kupoteza kikubwa ni kuona kwamba kila mmoja anatimiza majukumu yake.

Azam FC ambao ni mabingwa mara tano nao pia wanapaswa pongezi kwa kuwa wameonyesha ushindani licha ya kuishia hatua ya nusu fainali ya kwanza.