Home Uncategorized RUVU SHOOTING YAPIGA HESABU KALI MZUNGUKO WA PILI

RUVU SHOOTING YAPIGA HESABU KALI MZUNGUKO WA PILI

 


MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa kikosi chao kipo tayari kwa ajili ya mechi zao za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Ruvu Shooting ipo chini ya Kocha Mkuu, Charles Mkwasa ambaye ni mzawa akiwa ndani ya tano bora kwa msimu wa 2020/21. 

Kipo nafasi ya tano kwenye msimamo baada ya kucheza jumla ya mechi 17 ndani ya Ligi Kuu Bara na kibindoni kimekusanya jumla ya pointi 28.

Akizungumza na Saleh Jembe, Bwire amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya ushindani ndani ya ligi na wanaamini kwamba watafanya vizuri mzunguko wa pili.

SOMA NA HII  UONGOZI WA YANGA WAFUNGUKA UGUMU WA MECHI YA LEO DHIDI YA AZAM