Home Uncategorized SIMBA YATEMBEZA 4G KIMATAIFA, WIDA YAKUBALI KWA WAZIMBABWE

SIMBA YATEMBEZA 4G KIMATAIFA, WIDA YAKUBALI KWA WAZIMBABWE

 


KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck leo Januari 6 kimeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya FC Platinum kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika. 


Simba imepata matokeo hayo ikiwa nyumbani na kufanikiwa kupindua meza kibabe baada ya ule wa kwanza Zimbabwe kufungwa bao 1-0.


Bao la kwanza lilifungwa na Erasto Nyoni dakika ya 39 kwa mkwaju wa penalti baada ya Luis Miquissone kuchezewa faulo ndani ya 18 na mwamuzi kuamuru ipigwe penalti. 


Licha ya wachezaji wa FC Platinum kuonekana wakilalamika mwamuzi aliamuru ipigwe na bao la pili lilifungwa na Shomari Kapombe dakika ya 62.


Bao la tatu ilikuwa ni John Bocco dk 90+1 na msumari wa nne ni Clatous Chama kwa penalti dakika ya 90+5 na kuifanya Simba itinge hatua ya makundi.


Bao wakiwa ugenini walifungwa na Perfect Chikwende ambaye leo aliwekwa kwenye uangalizi wa Erasto Nyoni, Shomari Kapombe na Mohamed Hussein ambao walikuwa wakibadilisha kuweka ulinzi ndani ya Simba.

SOMA NA HII  UONGOZI WA YANGA WAFUNGUKA UGUMU WA MECHI YA LEO DHIDI YA AZAM