Home Uncategorized WANNE WA AZAM FC KUKOSA MAPINDUZI CUP

WANNE WA AZAM FC KUKOSA MAPINDUZI CUP


NYOTA watatu wa kikosi cha Azam FC watabaki Bongo kuendelea na majukumu yao katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars hivyo watakosekana kwenye mashindano ya Mapinduzi Cup.

 Wachezaji hao ni Ayoub Lyanga, Khleffin Hamdoun na beki wa kushoto, Pascal Msindo (U-20).


Kikosi cha Taifa Stars kinajiandaa na fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), zitakazofanyika kuanzia Januari 16 hadi Februari 7 mwaka huu nchini Cameroon.


Mbali na nyota hao watatu pia mshambuliaji namba moja Prince Dube mwenye mabao sita na pasi nne ndani ya Ligi Kuu Bara pia atakosekana kwenye Mapinduzi Cup kwa kuwa bado hajarejea kwenye ubora wake.

Leo Januari 5 kikosi cha Azam FC kinatarajiwa kuelekea Visiwani Zanzibar kwa ajili ya kushiriki Kombe la Mapinduzi.
SOMA NA HII  KESHO NI NAMUNGO V YANGA NI VITA YA KIBABE