Home kimataifa DI MARIA ABEBA MATUMAINI YA KUVUNJA REKODI YA SUSIC

DI MARIA ABEBA MATUMAINI YA KUVUNJA REKODI YA SUSIC

 


ANGEL Di Maria nyota wa Paris Saint-Germain, (PSG) amesema kuwa  matumaini yake makubwa ni kuona kwamba anavunja rekodi ya Safet Susic ambaye aliweza kutoa jumla ya pasi 103.

Di Maria mwenye miaka 33 ni raia wa Argentina aliibuka ndani ya PSG inayonolewa na Kocha Mkuu, Mauricio Pochetino akitokea Klabu ya Manchester United msimu wa 2015.

Amefunga jumla ya mabao 87 na ametoa pasi 99 ambazo zimeleta mabao jambo ambalo linamfanya azidi kuwa bora muda wote.

Ana deni la pasi nne kwa sasa ili aweze kufikia rekodi ya Susic ambaye aliwahi kucheza ndani ya Klabu ya PSG msimu wa 1982/1991. Rekodi zinaonyesha kuwa alicheza jumla ya mechi 287 na alitupia mabao 67.


SOMA NA HII  ORODHA YA MASTAA WANAOPIGIWA HESABU NA NEWCASTLE