Home Yanga SC FISTON: TULIAMBIWA MAPEMA KWAMBA TUNAFUNGWA ..!!

FISTON: TULIAMBIWA MAPEMA KWAMBA TUNAFUNGWA ..!!


 MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Yanga, raia wa Burundi, Fiston Abdulazack amesema kuwa suala la sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania wachezaji walifanya uzembe kwa kujisahau baada ya kutangulia kufunga.

Kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abed, Machi 7 ambao ulikuwa ni wa mwisho kwa benchi la ufundi lililokuwa likiongozwa na Cedric Kaze nyota huyo alifunga bao mapema.

Nyota huyo amesema kuwa mwalimu aliwaambia siku moja kabla ya mechi na hata siku ya mechi kwamba wamekuwa wakifungwa kwa mipira iliyokufa hivyo wanapaswa waongeze umakini.

Ilikuwa dakika ya 41 alifunga bao la utangulizi na kuwafanya Yanga waamini kwamba wamekamilisha kazi ya kusaka pointi tatu na dakika ya 89 Pius Buswita alifunga bao liliwatoa kwenye reli ya kusepa na pointi tatu.

Nyota huyo ambaye ni ingizo jipya ndani ya Yanga akiwa amesaini dili la miezi sita amesema kuwa wanaopaswa kulaumiwa kwa matokeo hayo ya sare ni wachezaji.

“Naweza kusema kwamba sisi wachezaji tunapaswa kulaumiwa kwa sababu ilikuwa ni furaha tukiamini kwamba tumeshinda ilihali bado tuna kazi ya kufanya kulinda na kuongeza bao jingine.

“Mwisho wa siku kujisahau kwetu kumetuponza licha ya kwamba mwalimu alituambia kwamba makosa yetu yapo kwenye mipira iliyokufa na tukafungwa kwa mipira iliyokufa,” amesema.

Kwa sasa Yanga ipo kwenye mchakato wa kumtafuta kocha mpya ambaye atakuja kurithi mikoba ya Kaze ambaye amekiacha kikosi kikiwa nafasi ya kwanza na pointi 50.

SOMA NA HII  YANGA YAAMBULIA KICHAPO CHA BAO 1-0 DHIDI YA AFRICAN SPORTS, CHAMAZI