Home FA Cup DODOMA JIJI: HATUTAKUBALI KUFUNGWA TENA NA SIMBA

DODOMA JIJI: HATUTAKUBALI KUFUNGWA TENA NA SIMBA


 MBWANA Makata, Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji amesema kuwa leo hawatakubail kupoteza mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba kwenye mchezo wao unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku.

Leo inakuwa ni mara ya tatu kwa timu hiyo kukutana na Simba katika mechi za ushindani kwa msimu wa 2020/21.

Mara ya kwanza ilikuwa ni kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma na ubao ulisoma Dodoma Jiji 1-2 Simba ule wa pili pia ulikuwa Uwanja wa Mkapa na ubao ulisoma Simba 3-1 Dodoma Jiji.

Leo ni wa tatu ila ni Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali na mshindi wa mchezo huo atatinga hatua ya nusu fainali ambapo atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Rhino Ranger ama Azam FC ambao wao watashuka Uwanja wa Kambarage saa 10:00 jioni.

Makata amesema:”Mara ya kwanza tulipoteza kwa kufungwa 1-2 na ule wa pili ilikuwa ni 3-1 sasa wakati huu yale makosa tumeyafanyia kazi na tunahitaji ushindi.

“Tutaingia uwanjani kwa heshima na nidhamu kwa kuwa tunajua tunacheza na timu kubwa na yenye wachezaji wakubwa ukizingatia kwamba wametoka kutolewa hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika,” amesema.

SOMA NA HII  ORODHA YA TIMU AMBAZO ZIMETINGA HATUA YA ROBO FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO