Home kimataifa MANCHESTER UNITED YAITAKA SAINI YA BEKI REAL MADRID

MANCHESTER UNITED YAITAKA SAINI YA BEKI REAL MADRID


IMEELEZWA kuwa Manchester United ipo kwenye hesabu za kuipata saini ya beki wa Real Madrid Raphael Varane ili kujiunga na timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solkjaer.

Baada ya United kukamilisha dili la winga Jadon Sancho ambaye amepewa dili la miaka mitano akitokea Klabu ya Borussia Dortmund ambaye ni winga na alikuwa anasakwa na mabosi hao kwa muda mrefu ila kikwazo awali ilikuwa ni dau kubwa walilokuwa wanataja mabosi wake hao.

Ripoti zimeeleza kuwa Varane yupo tayari kuondoka ndani ya Real Madrid msimu huu ili akapate changamoto mpya ambapo timu inayopewa nafasi upata saini yake ni Manchester United.

Florentino Perez ambaye ni Rais wa real Madrid anatajwa kuwa kikwazo namba moja kwa United kupata saini ya nyota huyo mwenye miaka 24 kwa kuwa ana hasira za kuikosa saini ya kiungo Paul Pogba ambaye alikuwa anatajwa kuibukia ndani ya kikosi cha Madrid.

SOMA NA HII  WAKATI TETESI ZIKISEMA ONYANGO ATATUA YANGA....MANARA AIBUKA NA KUMKATAA MCHANA KWEUPEE..