Home kimataifa MBAPPE ANATUZO KIBAO NA MABAO PIA

MBAPPE ANATUZO KIBAO NA MABAO PIA

 

NYOTA Kylian Mbappe anayecheza Klabu ya PSG amecheza jumla ya mechi 234 huku akifunga mabao 162.

Pia ametoa jumla ya pasi 79 katika mashindano yote ambayo amecheza. Katika Ligue 1 amecheza mechi nyingi ambazo ni 148 na amefunga mabao 107 na pasi 42.

Raia huyo wa Ufaransa alijiunga na PSG 2018 na mkataba wake unatarajiwa kumeguka Juni 2022.

Msimu huu katika Euro 2020 akiwa na timu yake ya taifa ya Ufaransa amecheza mechi nne na ametoa jumla ya pasi 2.

Ana tuzo ya kiatu cha dhahabu aliyopata mwaka 2017 pia ana tuzo tatu za mchezaji mdogo ndani ya Ligue 1 alizotwaa msimu wa 2016/17, 2017/18 na 2018/19 kwa sasa ana miaka 22.


SOMA NA HII  HAWA HAPA WACHEZAJI PEKEE WANAOIWAKILISHA TANZANIA KOMBE LA DUNIA QATAR...