Home Burudani MWISHO WA NYODO, MABONDIA WATAKA KUZICHAPA KAVUKAVU

MWISHO WA NYODO, MABONDIA WATAKA KUZICHAPA KAVUKAVU


MOTO wa pambano la mwisho wa nyodo  umepamba baada ya mabondia Hussein Itaba na Ibrahim Tamba kutaka kuzichapa kavukavu  kabla ya kuamuliwa kutokana na kurushiana baada ya kukutana kwa mara ya kwanza


Mabondia hao wamekutana jana kwenye Uwanja wa Las Vegas, Mabibo  ikiwa ni lengo la kutangaza pambano linalotarajia kupigwa Julai 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kinesi, Dar chini ya udhamini wa Global Tv online, gazeti la Championi, Creative Bee, Smart Gin, Good Hope Laboratory na Peak Time Media.


Katika tukio hilo ambalo lilitarajiwa kuhudhuiriwa na Dullah Mbabe kwa ajili ya kutangaza pambano lake dhidi ya Twaha Kiduku litakalopigwa Agosti 20, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza lakini hakuweza kutokea.


Lakini Itaba na Tamba walitaka kuzipiga kutokana na kila mmoja kumtambia mwenzake kwamba atampiga hali iliopelekea kutaka kuzichapa kabla ya kuamuliwa wakitakiwa kusubiria wakati wa pambano Jumamosi uweze kufika.


Wengine walizua tafrani ni Allya Ngwando na Omari Mpemba, Hassan Ndonga na Paul Magesta, Shomari Pendeza na Abdulrazack Kazumali.


Mabondia wengine watakaopanda ulingoni katika pambano la mwisho wa nyodo watakuwa ni  Khailu Makuti vs  Hassan Kagoma, Adam Chiga vs Simon Zibron, Hassan Ndoga vs Paul Magesta,

Lakini Julius Mpenda atazichapa na Abdallah Uyaga, Shomari Pendeza na Abdulrazak Kazumari, Omari Mpenda vs Ally Gonja, Boni Sela vs Ramadhan Kondo na Hafidh Mlawa vs Amour Zungu.


SOMA NA HII  MANARA ATANGAZA KUONGEZA MKE WA TATU..."NINA NGUVU...NITAWAHUDUMIA"...