Home Simba SC BREAKING:SIMBA YAMTANGAZA MCONGO MPYA, YEYE NI BEKI

BREAKING:SIMBA YAMTANGAZA MCONGO MPYA, YEYE NI BEKI


 KIKOSI cha Simba leo kimemtambulisha nyota mpya ambaye ni beki kutoka nchini Congo.

Ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Congo DR na beki kisiki, Henock Inonga Baka (26) ambaye kwa sasa ni mali ya Simba.

Kupitia ukurasa wao wa Instagram, Simba wameandika kwamba nyota huyo kwa sasa ni mali halali ya Simba.

Anakuwa nyota wa nne wa kigeni kutambulishwa Simba ambapo wa kwanza alikuwa ni Peter Banda raia wa Msumbiji kisha Duncan Nyoni na Pape Sokhu raia wa Senegal.

Timu hiyo imeweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2021/22 ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

SOMA NA HII  BREAKING: HAJI MANARA ABWAGA MANYANGA SIMBA, MBADALA WAKE HUYU HAPA