Home kimataifa TUCHEL ATAJA SABABU YA KUMPA DILI LUKAKU

TUCHEL ATAJA SABABU YA KUMPA DILI LUKAKU


KOCHA wa timu ya Chelsea, Thomas Tuchel amesema kuwa sababu kubwa ya kuhitaji saini ya Romelu Lukaku ni kupenda kwake kufunga jambo ambalo anaamini kwamba litamsaidia.

Lukaku anatua Chelsea akitokea Klabu ya Inter Milan ambapo huko alifanya vizuri msimu uliopita na kutwaa ubingwa wa ligi hiyo ndani ya Serie A.

Dau lake la usajili ni pauni milioni 97.5 ikiwa ni usajili wa ghali msimu huu ndani ya Ligi Kuu England baada ya ule wa kwanza kuwa ni wa Jack Grealish wa Manchester City ambaye alisajiliwa kwa pauni milioni 100 akitokea Aston Villa.

Tuchel amesema:”Nimemchagua Lukaku kwa sababu ni namba tisa halisi ambaye anapenda kufunga mabao. Anapenda kufunga akiwa na mpira amekuwa yuko vizuri lakini atasaidiwa kutengeneza nafasi na wachezaji kama Timo Werner, Kai Havertz na Christian Pulisic,” . 

SOMA NA HII  EPL, SERIE A NA LALIGA NI MWENDO MDUNDO