Home news FEI TOTO:HAIKUWA KAZI RAHISI, MAPAMBANO YANAENDELEA

FEI TOTO:HAIKUWA KAZI RAHISI, MAPAMBANO YANAENDELEA


FEISAL Salum, kiungo wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayonolewa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen amesema kuwa mchezo wao dhidi ya Madagascar haukuwa rahisi ila furaha yao ni kuona kwamba wamepata ushindi.


Septemba 7, Taifa Stars iliweza kupata ushindi wa mabao 3-2 na bao la ushindi lilifungwa na kiungo huyo wa mpira kwa mguu la kulia akimalizia pasi ya nahodha Mbwana Samatta.


Ushindi huo umeifanya Tanzania kuweza kuongoza kundi J kwa kuwa imefikisha jumla ya pointi 4 ikiwa sawa na ile ya Benin iliyo nafasi ya pili lakini tofauti ni kwenye idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Tanzania imefunga jumla ya mabao manne na Benin imefunga jumla ya mabao matatu, Madagascar ipo nafasi ya nne ikiwa haijakusanya pointi huku ile nafasi ya tatu ikiwa mali ya DR Congo.

Fei amesema:”Maelekezo ya mwalimu yamefanya kila kitu kiende vizuri, tunamshukuru Mungu tumepata ushindi, lakini haikuwa mchezo rahisi kwetu.

“Makosa ambayo tuliyafanya kipindi cha kwanza yalimfanya mwalimu kutuambia kwamba tunashindwa kumaliza nafasi na tunakaa sana nyuma jambo ambalo lilitufanya tubadilike kipindi cha pili na kupata ushindi,” 

Stars bado ina kibarua cha kufanya ili kuweza kupenya katika hatua ya makundi na kuwa miongoni mwa timu tisa ambazo zitakazocheza mchezo wa mtoano kwa ajili ya kusaka nafasi ya timu tano zitakazofuzu Kombe la Dunia nchini Qatar 2022.
SOMA NA HII  MAMA SAMIA AWAMWAGA MPUNGA...MIL 500 MEZANI...TAIFA STARS IKIFUZU AFCON

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here