Home news SIMBA YAPATA JEMBE LINGINE LA KAZI SASA

SIMBA YAPATA JEMBE LINGINE LA KAZI SASA


KIBU Dennis ingizo jipya ndani ya kikosi cha Simba sasa yupo huru kuitumikia Simba baada ya suala lake la vibali kukamilika na sasa rasmi ni raia wa Tanzania.

Kukamilisha kwa suala hilo sasa inakuwa rasmi Simba imepata jembe lingine la kazi kwa upande wa ushambuliaji ambao unaongozwa na nahodha mzawa, John Bocco, Meddie Kagere na Chris Mugalu hivyo anakuwa mshambuliaji wa nne.

Nyota huyo alikuwa hajaonekana katika mechi za awali za Simba kutokana na tatizo la uraia wake jambo ambalo lilipelekea pia jina lake kutokuwa katika orodha ya wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania,  Taifa Stars.

Taarifa ambayo imetolewa na Simba imeeleza kuwa yupo tayari kuitumikia Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ambaye anatajwa kukubali uwezo wake.

Pia taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani imeeleza kuwa kufuatia mamlaka aliyopewa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene kwa mujibu wa Sheria ya Uraia,Sura ya 357, (Rejeo la 2002) baada ya kupokea ombi lililoletwa kwake na TFF, amempa Uraia wa Tanzania mchezaji wa mpira wa miguu, Kibu Denis Prosper, Septemba 30,2021.

Kibu alikosekana kwenye mechi mbili za Simba ilikuwa mbele ya Biashara United na Dodoma Jiji.

SOMA NA HII  WAKATI YANGA WAKIWAZA UBINGWA KWANZA..NABI WALA HAFIKIRI HILO KUMBE...HIKI HAPA KIPAUMBELE CHAKE..