Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC, Ndugu Salim Mhene amemtangaza Mfanyabiashara mashuhuri nchini na Mwekezaji wa timu hiyo Ndg Mohammed Dewji kuwa Rais wa Heshima wa klabu hiyo kongwe nchini.
Mo Dewji ametangazwa hivi leo katika Mkutano Mkuu unaoendelea katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam, ambapo wanachama wameridhia kwa kauli moja.
Akitangaza uamuzi huo, Salim ‘Try Again’ amesema bodi ya timu hiyo ilikaa hivi karibuni ambapo kwa kuzingatia kanunia ya 50 Katiba ya Klabu hiyo, walimteua na kumpitisha kwa kauli moja Mo Dewji kwenye wadhifa huo mpya.
Aidha, Salim alisema kuwa , Wanachama na wapenzi wa Simba watulie kwani mambo makubwa yanakuja Simba.