Home Habari za michezo URAIS YANGA NI DK MSOLA Vs INJINI HERSI….MWAKALEBELA AEPUKA FEDHEHA YA KUSHINDWA…AMGEUKA...

URAIS YANGA NI DK MSOLA Vs INJINI HERSI….MWAKALEBELA AEPUKA FEDHEHA YA KUSHINDWA…AMGEUKA BOSI WAKE…


VITA ya kuwania nafasi za juu za uongozi wa klabu ya Yanga imepambana moto baada ya jana Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya klabu hiyo, Injinia Hersi Said amerudisha rasmi fomu hiyo akiutaka urais, huku kwenye umakamu mwenyekiti nako ni moto mkali.

Uchaguzi Mkuu wa Yanga umepangwa kufanyika Julai 10 ili kupata viongozi wa kuchukua nafasi ya wanaomaliza muda wao wakiongoza na Dk Mshindo Msolla na makamu wake, Fredrick Mwakalebela.

Hersi anakuwa mgombea wa pili kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ya juu katika mabadiliko mapya ya uongozi wa Yanga, kwani mapema Mwenyekiti wa sasa wa klabu hiyo Dk Mshindo Msolla alikuwa wa kwanza kuchukua fomu.

Hersi jana alirudishiwa fomu hiyo na mmoja wa rafiki zake makao makuu ya klabu ya Yanga, huku akisindikizwa na makundi ya wanachama na mashabiki wa klabu hiyo wakiwa pia na kikundi cha ngoma.

Katika msafara wa Hersi pia alikuwemo Makamu Mwenyekiti wa uongozi wa sasa, Fredrick Mwakalebela na alisema ameamua kutogombea nafasi hiyo huku akiwa upande wa kambi ya Hersi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM wanaoidhamini klabu hiyo.

“Nimekuwa katika uongozi ambao tunaondoka kwa mafanikio, lakini kuondoka kwangu ni lazima tuiache klabu katika mikono salama na mimi usalama huu nauacha kwa mgombea huyu (Hersi) ambaye nina imani naye kubwa,” alisema Mwakalebela.

Wakati Hersi akichukua fomu ya urais upande wa makamu wa rais kulikuwa na jina moja tu la Arafat Haji aliyechukuliwa na fomu kisha kurudishwa.

Arafat ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Shirikika la Bima la Zanzibar alichukuliwa fomu hiyo na wanachama na mashabiki licha ya awali kutangaza kutogombea kutokana na kuwa sehemu ya uongozi wa sasa wa Dk Msolla.

Mpaka jana Arafat alikuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo, huku Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Ally Mchungahela alisema kuwa zoezi hilo la kuchukua fomu na kurudisha sasa litafungwa jana Juni 10 na uchaguzi huo utafanyika Julai 10.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA MAMBO MAGUMU...YANGA WAAZIMA WACHEZAJI SIMBA ILI WAFUZU CAF...

“Tumeona tusogeze mbele kwa siku moja zoezi hili la kuchukua fomu na kurudisha kutokana na siku ambayo tulianza, ilikuwa ni Juni 5 ambayo ilikuwa siku ya mapumziko, tukasema tuwape nafasi wanachama kujitafakari kuliko kuwakimbiza,” alisema Mchungahela.