Home Habari za michezo KAMWE: TUMEPOKELEWA NA WAPINZANI WAO…WAMETUAMBIA HAWATISHI SANA TUSIWE NA WASIWASI…

KAMWE: TUMEPOKELEWA NA WAPINZANI WAO…WAMETUAMBIA HAWATISHI SANA TUSIWE NA WASIWASI…

Habari za Yanga

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kikosi chao kilipokelewa vizuri nchini Tunisia ambapo sasa kinajiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya Club Africain kwa ajili ya kusaka tiketi ya kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

“Tangu tumefika hapa tumepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa klabu ya Etoile du Sahel (wapinzani wa Club Africain) ambao wametuambia kuwa Club Africain sio wa kutisha kwa sasa kwa kuwa pia wana BAN (Wamefungiwa) na FIFA.

“Mpaka sasa hakuna changamoto yoyote, hali ya hewa huku ni baridi ndio maana tuliondoka mapema ili kuizoea hali ya hewa,” alisema Ally Kamwe.

SOMA NA HII  KIUNGO AZAM FC AFUZU MAJARIBIO LIVERPOOL