Home Habari za michezo IMEFICHUKA….MSHAHARA WA NTIBAZONKIZA SIMBA SC NI KUFURU TUPU…

IMEFICHUKA….MSHAHARA WA NTIBAZONKIZA SIMBA SC NI KUFURU TUPU…

Usajili wa dirisha dogo unazidi kutikisa nchini baada ya dirisha dogo kufunguliwa rasmi Desemba 15, 2022. Wekundu wa Msimbazi Simba SC, wamtambulisha rasmi Kiungo Mshambuliaji raia wa Burundi, Saido Ntibanzokiza.

Kupitia ukurasa wao, Simba wametupia picha ya nyota huyo aliyekuwa akiitumikia Geita, na kumtambulisha kama mchezaji wao mpya.

Saido ataungana na mastaa wengine wa Simba SC kama Clatous Chama, Moses Phiri, Agustine Okrah, Pape Sakho na wengineo kuongeza nguvu katika eneo la ushambuliaji.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu kutoka Simba SC, Ntibazonkiza amelipwa Milioni 50 za usajili pamoja na mshahara wa Dola 3500 sawa na zaidi ya Milioni 8 kwa mwezi.

Ukipiga hesabu kwa mshahara huo, Simba SC italazimika kumlipa zaidi ya Milioni 192 kwa muda wote wa mkataba wake wa miaka miwili kama sehemu ya mshara tu

Mbali na hivyo, pia Saido amepangiwa nyumba ya kisasa pamoja na kupewa gari kwa ajili ya matumizi yake binafsi, hii inakwenda sambamba na posho za ushindi endapo timu itashinda kwenye mechi mbalimbali.

Simba wamesema wanatarajia kuongeza wachezaji wawili au watatu kwenye dirisha dogo linalotarajiwa kufungwa Januari 15, 2023.

SOMA NA HII  KWA HALI JINSI ILIVYO...YANGA WAKIZUBAA KIDOGO TU ..IMEKULA KWAO MAZIMA...ISHU IKO HIVI 'MWAMBA'...