Home Habari za michezo KOCHA TAIFA STARS:- NATEGEMEA UGANDA WATABADILIKA KATIKA MECHI HII…LAZIMA WAFE KIFO CHA...

KOCHA TAIFA STARS:- NATEGEMEA UGANDA WATABADILIKA KATIKA MECHI HII…LAZIMA WAFE KIFO CHA MENDE

Taifa Stars

KAMBI ya timu ya taifa, Taifa Stars imezidi kunoga baada ya mabeki wawili wa pembeni wa Simba, Shomary Kapombe na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kuongezwa kikosi hicho kwa mechi dhidi ya Uganda, huku kocha mkuu wa timu hiyo akitamba kwamba The Cranes itakufa tena Kwa Mkapa.

Kapombe na Tshabalala wameitwa kwenye timu timu hiyo baada ya awali kutojumuishwa Stars ilipoenda Misri kucheza mechi ya kwanza dhidi ya Uganda ikiwa ni pambano la Kundi F la kuwania Fainali ya Kombe la Afrika (Afcon) litkalofanyika mwakani nchini Ivory Coast.

Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia ndiye aliyetangaza kurejeshwa kwa mabeki hao Stars katika mkutano uliofanyika jana jijini Dar es Salaam na kufafanua ni pendekezo la kocha Adel Amrouche na kwamba tayari wapo kambini kwa sasa.

Awali kuachwa kwa mabeki hao kulizua mijadala na madai kwamba huenda kikosi hicho hakikuitwa na kocha huyo kutokana na umahiri na uzoefu walionao wachezaji hao kwa mechi hiyo ambayo Stars ilishinda 1-0 na kesho Jumanne watarudiana nao Kwa Mkapa, huku Amrouche akiitabia Uganda.

“Maneno yalikuwa mengi sana baada ya uteuzi uliofanyika mwanzoni, lakini tumeona matunda yake, kuongezwa kwa Kapombe na Tshabalala ni pendekezo la kocha. Sisi hatuwezi kuingilia majukumu yake kwani tunaamini katika weledi aliokuwa nao, jukumu kubwa kwetu ni kuendelea kumpa ushirikiano ili kwa pamoja tufikie malengo yetu kama taifa,” amesema Karia.

Mapema kocha wa timu hiyo, Adel Amrouche alisema anategemea kuiona Uganda ikibadilika kwenye mchezo huu, lakini hilo haliimpi shida kwa kuamini ubora wa kikosi alichonacho na kwamba anaamini watapata matokeo mazuri kwa mara nyingine na kujiweka pazuri kundini.

Amrouche alisema licha ya kuwa na siku chache za kujiandaa atatumia udhaifu aliouona kwa Uganda kuimaliza tena nyumbani, huku akisema anafanyia kazi maboresho ya kimbinu kwenye kikosi cha Stars kilicho na maingizo mengi mapya ambayo yanaweza kuwa na tija kwa taifa kwa siku za usoni.

“Tunatakiwa kucheza kitimu zaidi ili tufikie lengo, nidhamu ni jambo muhimu kwenye kushambulia na kuzuia, ninafuraha kuwa na wachezaji wenye kujitoa na kuwa na njaa ya mafanikio, tuwape sapoti, tuwaunge mkono kwa sababu wapo kwa ajili yetu,” alisema Amrouche.

Katika kuongeza mzuka kwa mastaa wa timu hiyo serikali kupitia Rais Samia Suluhu Hassan imeahidi kulipa Sh 10 Milioni kwa kila bao litakalofungwa kwenye mchezo huo na ijayo ya kundi hilo, huku ikifuzu kwenda Ivory Coast itavuna Sh 500 Milioni.

Pia Rais Samia amechangia tiketi 7,000 kwa mashabiki, wakati Wairi Mkuu amechangai 2000 na Wizara wa Michezo kupitia Katibu Mkuu wake, Said Yakubu imesema itachangia 11,000 ikiwamo na wadau wengine ambao hawakutaka kutajwa ili kuongeza hamasa kwa mchezo huo.

Stars iliyo na pointi nne kwa sasa ikishika nafasi ya pili nyuma ya Algeria yenye pointi tisa, kama itashinda mechi hiyo ya kesho itaifanya ifikishe pointi saba na kujiweka pazuri kwa safari ya Afcon ya tatu baada ya zile za awali za mwaka 1980 na 2019 zilizofanyika Nigeria na Misri mtawalia.

SOMA NA HII  HATIMAYE WAPINZANI WA SIMBA...KLABU BINGWA...WAANZA SAFARI KUTUA DAR