Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA SIMBA NA YANGA…HUU HAPA UDHAIFU WA WATANI WA JADI

KUELEKEA MECHI YA SIMBA NA YANGA…HUU HAPA UDHAIFU WA WATANI WA JADI

KUELEKEA MECHI YA SIMBA NA YANGA...HUU HAPA UDHAIFU WA WATANI WA JADI

Kocha na nyota wa zamani wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa ameuangalia ubora wa timu yake hiyo ya zamani na ule wa Simba na kutoa tathimini ya mechi yao ya Jumapili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Licha ya kuwataja Clatous Chama na Fiston Mayele katika mchezo huo, Mkwasa alisema ubora wa Simba unakuwa zaidi kwa washambuliaji, wakati Yanga itatawala kwenye beki katika mechi hiyo

“Japo mara nyingi dabi hizi huwa na ufundi mdogo, kwa kuwa kuna kukamiana na presha kubwa kutoka kwa mashabiki, ila ni mechi ngumu na kila upande una nafasi ya kufanya vizuri.

“Kitakachoamua matokeo ni namna kila timu itakavyojipanga, mikakati ya kila timu na namna kila moja itakavyofanikiwa kuzuia, kukaba na wepesi wa wachezaji.

“Timu zote mbili zina wachezaji wazuri, wako ‘dynamic’ (wana nguvu) kwa Yanga Mayele ukimuachia kidogo tu anakufunga, Simba kina Chama wanaweza kutengeneza mipango ya ushindi.

“Hapo ni namna ya kuthibitiana, timu itakayozubaa inafungwa, ingawa ukiangalia Simba wana wachezaji wazuri mbele, wenye uwezo wa kufunga na hawana mtu maalumu wa kufunga, yeyote anaweza kufunga.

“Udhaifu wao upo kwenye beki hasa katika ukabaji, kocha anapaswa kufanya kazi ya ziada kwenye hilo kwani kuna watu wanaonekana hawana wepesi wa kuona makosa na kurekebisha kwa haraka,” alisema Mkwasa.

Alisema Yanga ina viungo wazuri, japo kwenye kufunga, inamtegemea zaidi mtu mmoja, ambaye kama atadhibitiwa itakuwa ni kazi ya ziada. “Ukiangalia wafungaji, Yanga anaongoza Mayele (mabao 16), anayemfuatia kuna pengo kubwa (hadi kwa Aziz Ki mabao nane), wakati Simba ni Moses Phiri (10), John Bocco (9), Pape Ousmane Sakho na Jean Baleke (7),” alisema.

SOMA NA HII  KWA HILI GAMONDI AMPE HEKO KAZE