Home Habari za michezo ULE MGOLI WA INONGA UMEANDIKA REKODI HII…UMEVUNJA REKODI YA OKWI

ULE MGOLI WA INONGA UMEANDIKA REKODI HII…UMEVUNJA REKODI YA OKWI

Habazi sa Simba na Yanga

BAO la kwanza lililofungwa jana na beki wa kati Henock Inonga, limeingia kwenye rekodi ya mabao ya haraka kufungwa kwenye Kariakoo Derby, akifuata nyayo za Emmanuel Okwi aliyefanya hivyo mwaka 2012.

Simba na Yanga zilivaana jana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam katika pambano la 110 la Ligi Kuu Bara tangu mwaka 1965 na Wekundu kuibuka na ushindi wa mabao , huku Inonga akiitanguliza kwa bao la dakika 1 na sekunde 43.

Beki huyo kutoka DR Congo alifunga bao hilo kwa kichwa akimalizia krosi ya Shomary Kapombe aliyeanzishiwa kona fupi na Inonga kuruka hewani mbele ya mabeki wa Yanga na kumtungua kipa Djigui Diarra.

Huyo anakuwa beki wa kati wa pili wa Simba kufunga kwenye derby kwa miaka ya karibuni baada ya Joash Onyango aliyefunga kwenye pambano la Nov 07, 2020 ambalo liliisha kwa sare ya 1-1, beki huyo Mkenya akichomoa bao la Yanga lililowekwa kimiani na Michael Sarpong.

Tangu mwaka 2012, bao la Okwi lililofungwa kwenye pambano la watani lililpigwa Mei 6 na Simba kushinda mabao 5-0, ndilo lililokuwa la mapema zaidi, akifunga dakika ya kwanza.

SOMA NA HII  UBABE WA YANGA WAIHAMISHA GEITA GOLD