Home Habari za michezo ALLY KAMWE AJITWIKA ZIGO LA ZILIPO BILIONI 1.5 ZA JEZI….AFUNGUKA MIL 300...

ALLY KAMWE AJITWIKA ZIGO LA ZILIPO BILIONI 1.5 ZA JEZI….AFUNGUKA MIL 300 ILIYOSEMWA NA INJINIA HERSI…

Afisa Habari wa Yanga SC Ally Kamwe

Wakati Taarifa zikisamba na kuonesha kuwa Klabu ya Yanga imepata faida ya Tsh Milioni 300 kutokana na mauzo ya jezi zikionekana kuwashangaza wengi.

Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe ameondoa sintofahamu hiyo kwa kufafanua nini kipi hasa kilichomaanishwa wakati wa ufafanuzi wa Faida iliyopatikana kulingana na mauzo ya jezi ya Klabu ya Yanga.

Akizungumza Ally Kamwe amesema;

“Watu wanachanganya mambo, Yanga iliingia Mkataba wa Jezi na GSM wenye thamani ya Bilioni 1.5, sasa sisi kama Klabu tuliamua kununua jezi kwa bei ya Jumla kutoka kwa GSM na kuamua kuuza katika duka letu la Klabu pale jangwani”

“Sasa faida tuliyopata kutokana na mauzo ya jezi ya duka letu la klabu ndio hiyo unayoisema lakini ile Bilioni 1.5 iko palepale.

SOMA NA HII  YANGA YAWAITA WANACHAMA KWA WINGI KUWA SEHEMU YA HISTORIA