Home Habari za michezo KUHUSU NANI MFUNGAJI BORA…BODI YA LIGI WAINGILIA KATI UBISHI WA MAYELE NA...

KUHUSU NANI MFUNGAJI BORA…BODI YA LIGI WAINGILIA KATI UBISHI WA MAYELE NA NTIBAZONKIZA..

Habari za Michezo

Hatma ya tuzo ya mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu huu, itatolewa na kamati ya tuzo ya Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), muda wowote kuanzia sasa.

Ofisa Habari ya Bodi ya Ligi, Karim Boimanda amesema kwamba; “Kamati ya tuzo ya TFF itatoa uamuzi muda wowote kuanzia sasa.” Alifafanua Ofisa huyo bila kutaja muda maalum wa uamuzi huo.

Kauli hiyo imetokea baada ya msimu wa 2022/2023 kumalizika jioni hii huku Fiston Mayele wa Yanga na Saido Ntibanzokiza wa Simba kumaliza na mabao 17 kila mmoja huku kanuni zikiwa hazitoi suluhu.

Saido alifunga mabao hayo akiwa na timu mbili tofauti ambapo sita aliyafunga akiwa na Geita Gold na mengine 11 kuyafunga akiwa na Simba aliyojiunga nayo katika dirisha dogo la usajili.

Mayele amefunga mabao yote 17 akiwa na Yanga aliyojiunga nayo msimu wa 2021/2022 kipindi ambacho pia Saido alikuwa mchezaji wa timu hiyo yenye masikani yake mitaa ya Jangwani Dar es Salaam.

Idadi hiyo ya mabao (17) ni sawa na aliyokuwa nayo mfungaji bora wa msimu uliopita, George Mpole wakati akichezea Geita Gold ambapo nyuma yake alikuwepo Mayele aliyefunga 16.

Saido ndiye mchezaji aliyehusika na mabao mengi zaidi msimu huu 29, akifunga 17 na kutoa pasi za mwisho 12 akifuatiwa na Mayele aliyehusika kwenye mabao 20, akifunga 17 na asisti nne.

Kwa maana hiyo, kama TFF itafuata kanuni za Fifa wawili hao, Saido na Mayele watatwaa tuzo ya ufungaji bora ambapo kila mmoja atapewa kiatu chake.

SOMA NA HII  YANGA KWAMBINDE SANA DHIDI YA NAMUNGO, MUDATHIR AFANYA MIUJIZA