Home Habari za michezo KUHUSU AZAM FC…ONYANGO AANIKA KILA KITU WAZI….AFUNGUKA MIPANGO ILIVYOKUWA…

KUHUSU AZAM FC…ONYANGO AANIKA KILA KITU WAZI….AFUNGUKA MIPANGO ILIVYOKUWA…

Tetesi za Usajili Simba

Beki wa Simba SC, Joash Onyango amesema kufanya vibaya kwa timu yake msimu huu kumechangiwa sana na Azam FC kwa kupoteza mechi zote mbili muhimu walipokutana nao.

Onyango raia wa Kenya pia amekanusha taarifa kuwa baada ya mechi dhidi ya Wydad Casablanca nchini Morocco aliandika barua ya kuondoka kwenye klabu hiyo, na wala hana taarifa za kutakiwa na klabu yake ya zamani, Gor Mahia.

Beki huyo aliyesajiliwa na Simba akutokea Gor Mahia ya Kenya mwaka 2019 alisema mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya mzunguko wa kwanza dhidi ya Azam FC walipofungwa bao 1-0 iliwaondoa kwenye reli ya kuwania ubingwa, lakini pia mechi ya nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ dhidi ya timu hiyo hiyo ilipofungwa mabao 2-1, iliwachanganya zaidi na kuhitimisha mwisho wao wa kutoka bila kombe lolote msimu huu.

“Mechi hii ya majuzi tuliyotolewa na Azam kwenye nusu fainali Kombe la FA haikuwa picha nzuri kwetu wachezaji, ilituuma sana, kwa sababu ndiyo nafasi tuliyokuwa tumebaki nayo angalau na sisi msimu huu tupate kombe, na kwenye Ligi Kuu pia tulipopoteza mechi dhidi ya Azam nayo ndiyo iliyotutoa kabisa kwenye mfumo na kwenye reli na hasa mbio za kuwania ubingwa, kwa hiyo niseme hizi mechi mbili tulizocheza nao zimetufanya tupoteze mataji msimu huu,” amesema Onyango.

Mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu kati ya timu hizo ilichezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 27, Azam ikishinda bao 1-0, lililofungwa na Prince Dube na ile ya nusu fainali ya Kombe la FA, ilichezwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara, Mei 7, Simba ikipoiteza kwa mabao 2-1 ya Dube na Lusajo Maikenda, Sadio Kanoute akiifungia timu hiyo bao la kufutia machozi.

Pia Beki huyo wa kati anayeichezea pia timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars alinanusha taarifa kuwa aliandika barua ya kuondoka kwenye klabu hiyo baada ya mechi dhidi ya Wydad Casablanca.

“Binadamu huwezi kumzuia kusema, hata maiti inasemwa, yaani kuna mtu anaonekana kunifahamu mimi zaidi kuliko ninavyojifahamu, mambo yamekuwa mengi sana, mara nimesema hili, lakini mimi sikuwahi kutoa taarifa yoyote ya kuondoka, maana baada ya mechi na Wydad nikasikia maneno mengi, eti naomba kuondoka, si kweli, mimi bado nina mkataba wa Simba, mabosi wenyewe kama wataamua kuvunja sawa, sijasaini kuichezea maisha, huu ni mkataba tu, unaweza kuvunjwa, na kama ukiisha ukiongezwa sawa tu,” amesema

SOMA NA HII  SIMBA: MTIBWA SUGAR HUWA WANATUPA CHANGAMOTO,