Home Habari za michezo AHAMED ALLY ATAMBA AWAAMBIA MANENO HAYA MASHABIKI

AHAMED ALLY ATAMBA AWAAMBIA MANENO HAYA MASHABIKI

Habari za Simba SC

Mpira wa miguu kilele chake huwa ni ushindi (kupata alama tatu au kwenye mashindano ni kufuzu hatua inayofuata), kwenye Ligi tumechukua alama tatu dhidi ya Mtibwa Sugar, Dodoma Jiji na Coastal Union.

Kwa hiyo ukija kwenye malengo, bado tupo kwenye malengo ambayo ni kushinda mechi kadiri tuwezavyo. Watu wanataka timu ifunge magoli mengi, msimu uliopita tulifunga magoli mengi na hatukuwa mabingwa.

Huyu ambaye anasema tunashinda lakini hatuna furaha, itakuaje kama tutaendelea kushinda na kuwa mabingwa, atakuja kusema hana furaha ya ubingwa? Acha tuendelee kuishi kwenye malengo makuu ambayo ni kushinda kila mechi.

SOMA NA HII  WAKATI SIMBA NA YANGA ZIKIJIMWAYA MWAYA ...WAZO LA UJENZI WA UWANJA WA MKAPA LILITOKA HAPA...